FAHAMU SIRI ILIYOPO NYUMA YA FIZI KUVIMBA
FAHAMU SIRI ILIYOPO NYUMA YA FIZI KUVIMBA
Oct. 12, 2024

FIZI KUVIMBA (GINGIVITIS)

Fizi kuvimba (kitaalamu Gingivitis) ni tatizo la kiafya ambalo hujitokeza kinywani na kuathiri fizi kupelekea kua laini,kubadilika rangi, kutoa damu na hata maumivu makali. Ugonjwa huu ni wa kawaida na mtu yeyote anaweza kuupata. Mara nyingi huwapata watu katika umri wa balehe na katika nyakati tofauti tofauti pia katika maisha.

Kwa nini fizi zinavimba?

Kutokuwa na tabia ya kufanya usafi wa kinywa na meno kama inavyoelekezwa na wataalam wa Afya..

Ugaga (Utando mgumu kwenye meno unaosababishwa na mabaki ya chakula kukaa kwa muda mrefu kinywani).

Maambukizi ya bakteria, virusi ama fangasi kinywani.

Mzio (Allergy) kutokana na vyakula ama vinywaji pamoja na matumizi ya baadhi ya dawa za meno.

Mabadiliko ya homoni wakati wa balehe, mzunguko wa hedhi, mimba ama ukomo wa hedhi.

Matumizi ya tumbaku na sigara.

Athari za magonjwa kama Kisukari na VVU/UKIMWI.

Matumizi ya dawa hasa dawa za presha ama kifafa.

Upungufu wa vitamin C (Vitamini  hupatikana kwenye Machungwa, Nyanya, Pilipili, Viazi n.k).

Uzee.

Dalili za fizi kuvimba ni zipi? 

Fizi kutoa damu wakati wa kupiga mswaki ama kung’ata kitu.

Ufizi kuwa na rangi nyekundu zaidi tofauti na rangi ya pinki iliyopauka ambayo ni rangi ya kawaida kwa ufizi wenye afya imara.

Maumivu kwenye fizi (hii huwapata wachache).

Fizi kuchubuka kwa urahisi na kusababisha vidonda kwenye fizi, kama tatizo limekaa kwa muda mrefu bila kutibiwa.

Harufu mbaya mdomoni.

Nifanyeje ili niweze kuepukana na matatizo ya fizi KUVIMBA?

Ili kuepuka tatizo la Gingivitis, piga mswaki angalau mara pili kwa siku (baada ya kunywa chai na baada ya chakula cha jioni) kwa kutumia mswaki laini na dawa ya meno. 

Muone daktari wako wa Kinywa na Meno angalau mara mbili kwa mwaka ili kutambua maradhi ya kinywa kama unayo.

Ili kuondoa athari na dalili ambazo zimesababishwa na gingivitis, tumia dawa inayoitwa CERVITEC GEL. Dawa hii huua viini vya bakteria hatarishi kinywani na  hutibu na kuondoa uvimbe na dalili zote za gingivitis na pia huondoa kabisa tatizo la harufu mbaya

WhatsApp