VIDONDA VYA KINYWANI (RECURRENT APHTHOUS ULCERS)
Hivi ni vidonda vya kinywani vinavyojitokeza kwenye utando wa fizi na midomo ya juu na chini. Pia hujulikana kwa jina la “Canker Sores”. Vidonda hivi huwa vina umbo la mviringo na rangi ya njano au nyekundu na hutokea sehemu laini kinywani kama vile upande wa ndani wa midomo (lips), sehemu ya ndani ya mashavu na chini ya ulimi.
Vidonda hivi siyo vya kuambukizwa, na huweza kutokea kama kidonda kimoja ama vikawa vingi vingi. Hua na tabia ya kujirudiarudia na ndiyo maana vikaitwa kwa lugha ya kitaalamu “Recurrent Aphthous Ulcers”. Vikitokea hudumu kwa siku 7 hadi 10 na vinakuwa vimeambatana na maumivu makali.
Visababishi vya vidonda vya kinywani
Hakuna chanzo rasmi kinachojulikana hadi sasa japo kuna baadhi tu ya visababishi ambavyo hua vinakisiwa kua ndiyo chanzo haswa.
-Msongo wa mawazo (sonona)-kisababishi kikuu.
-Jeraha mdomoni kutokana na kujing’ata,kupiga mswaki kwa nguvu au meno ya bandia yaliyokaa vibaya kinywani.
-Historia ya ugonjwa katika familia
-Upungufu wa vitamin b 12 na madini ya chuma
-Mabadiliko ya homoni wakati wa balehe ama ujauzito
-Upungufu wa kinga mwilini (kinga kuwa dhaifu).
Matibabu
Mpaka sasa hakuna tiba ya vidonda vya kinywani inayojulikana. Vidonda hivi mara nyingi hupotea bila matibabu. Hata hivyo, kutokana an maumivu makali yanayosababishwa na vidonda hivi, kuna njia mbalimbali za kuzuia na kuondoa dalili.
Matumizi ya dawa mchanganyiko wa Triamcinolone+Lidocaine kupunguza maumivu. Dawa hii hupakwa kwenye vidonda hivyo.
Kutumia dawa ya kusukutua kama vile Chlorhexidine,kila baada ya kupiga mswaki.
Antibiotiki kama vile Tetracycline a Minocycline