1.FANGASI ZA KINYWA (ORAL CANDIDIASIS)
Fangasi za kinywa, pia hujulikana kama oral thrush au candidiasis ya kinywa, ni maambukizi yanayosababishwa na kuongezeka kwa fangasi aina ya Candida albicans ndani ya kinywa. Fangasi hawa kawaida huishi ndani ya kinywa bila kuleta madhara, lakini wanapoanza kuzaliana kupita kiasi, maambukizi hujitokeza.
Sababu za kushambuliwa na Fangasi za Kinywa:
Matumizi ya dawa za antibiotiki kwa muda mrefu bila kusitisha:Antibiotiki zinaweza kuua bakteria wazuri ambao huzuia kukua kwa fangasi,hivyo kuruhusu fangasi kuongezeka.
Matumizi ya dawa za steroidi: Steroidi, hasa zile zinazotumiwa kwa kuvuta (inhalers), zinaweza kuchangia maambukizi ya fangasi kinywani.
Upungufu wa kinga mwilini: Watu wenye kinga dhaifu ya mwili, kama wagonjwa wa kisukari, VVU/UKIMWI, au wanaopata matibabu ya saratani, wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa.
Matumizi ya meno bandia(dentures):Meno bandia,hasa kama hayajafungwa vizuri au yasipotunzwa vizuri, yanaweza kutoa mazingira mazuri kwa ukuaji wa fangasi.
Matatizo ya kinywa kikavu: Upungufu wa mate unaweza kusababisha fangasi kukua kwa wingi kwa sababu mate husaidia kuzuia ukuaji wa fangasi.
Lishe duni au utapiamlo: Upungufu wa virutubishi kama chuma, vitamini B12, au asidi ya foliki huongeza uwezekano wa kupata fangasi za kinywa.
Matumizi ya sigara na tumbaku: Kuvuta sigara na tumbaku huongeza hatari ya kuambukizwa fangasi kinywani.
Dalili za Fangasi za Kinywa:
Michubuko au matabaka (layer) meupe kwenye ulimi au mashavu ya ndani: Michubuko hii inaweza kuonekana pia kwenye fizi, paa la kinywa, au koo.
Kupoteza ladha:Watu wenye fangasi za kinywa wanaweza kuhisi mabadiliko ya ladha au kupoteza ladha kabisa.
Kupasuka kwa ngozi kwenye kona za midomo: Midomo inaweza kuwa na michubuko au kupasuka kwenye kona za midomo (angular cheilitis).
Ugonjwa wa fizi au damu kutoka kwenye fizi: Hii inaweza kutokea kwenye maeneo yaliyoathirika na fangasi.
Maumivu wakati wa kumeza: Ikiwa maambukizi yamesambaa hadi kwenye koo, inaweza kusababisha maumivu wakati wa kumeza.
Matibabu ya Fangasi za Kinywa:
Dawa za antifungal: Hizi ni dawa za kuua fangasi kama vile nystatin, fluconazole, au clotrimazole, zinazotumika kama vidonge, lozenges, au madoido ya kinywa.
Marekebisho ya meno bandia: Kama meno bandia yanasababisha maambukizi, yanaweza kuhitaji kurekebishwa au kusafishwa vizuri zaidi.
Matumizi sahihi ya inhalers: Kwa watumiaji wa dawa za kuvuta (inhalers), ni muhimu kusafisha kinywa kwa maji baada ya kila matumizi ili kupunguza hatari ya fangasi.
Marekebisho ya lishe: Lishe bora iliyo na vitamini na madini muhimu kama chuma, vitamini B12, na foliki asidi inaweza kusaidia kuimarisha kinga ya mwili na kupunguza hatari ya fangasi.
Matibabu ya magonjwa yanayohusiana: Kama kuna ugonjwa wa msingi unaochangia maambukizi ya fangasi (kama kisukari au VVU), matibabu ya ugonjwa huo ni muhimu ili kuzuia maambukizi ya mara kwa mara.
Namna ya kujiepusha na Fangasi za Kinywa:
Usafi bora wa kinywa: Safisha meno mara mbili kwa siku na hakikisha unatumia dawa ya meno yenye madini ya fluoride. Safisha pia ulimi mara kwa mara.
Epuka matumizi ya kupindukia ya antibiotiki: Tumia dawa za antibiotiki kwa uangalifu, na ni bora tu baada ya kupata ushauri wa daktari.
Safisha meno bandia vizuri: Weka meno bandia katika hali nzuri ya usafi, sugua vizuri kila siku, na vaa kwa namna inayofaa.
Tumia dawa za steroidi kwa uangalifu: Ikiwa unatumia dawa za kuvuta za steroidi, sugua kinywa kwa maji baada ya kila matumizi ili kuzuia fangasi kukua.
Jiepushe kutumia tumbaku na sigara: Kuvuta sigara kunaongeza hatari ya kupata maambukizi ya fangasi. Kuacha kuvuta sigara ni moja ya njia bora za kujikinga.
Kwa kufuata ushauri wa kiafya na kuwa na usafi wa kinywa mzuri, unaweza kupunguza hatari ya kuambukizwa fangasi za kinywa na kudumisha