CERVITEC FLUID & GEL
Cervitec Fluid na Cervitec Gel ni bidhaa za utunzaji wa meno na kinywa zinazotengenezwa na Ivoclar Vivadent, kampuni inayojulikana kwa utengenezaji wa vifaa na bidhaa za meno.Kwa Tanzania Dentopharma ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa hizi.
Zina chlorhexidine na fluoride, viambato viwili ambavyo vina uwezo wa kuzuia maambukizi ya bakteria na kuimarisha meno dhidi ya kuoza.Hizi bidhaa hutumika kwa matibabu ya kitaalamu na pia nyumbani chini ya usimamizi wa daktari wa meno.
(a)Cervitec Fluid:
Cervitec Fluid ni dawa ya maji inayotumiwa kutibu na kudhibiti maeneo yenye hatari ya maambukizi ya bakteria kwenye kinywa.Hii ni jamii ya mouth wash ambayo haina viambata hai vya kilevi (alcohol-free).
Dawa hii hutumika kusukutua kwa sekunde 30-60 baada ya kupiga mswaki kwa dawa yenye madini ya floridi.Unashauriwa kutema dawa yote baada ya kusukutua bila kusuza na maji ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Matumizi:
Kusafisha kinywa nyumbani au kliniki kwa daktarin wa kinywa na meno
Hutumika kwa wagonjwa walio na maambukizi ya fizi (gingivitis na periodontitis).
Inafaa kwa wagonjwa walio na hatari kubwa ya kuoza meno kutokana na uwepo wa implants, taji bandia ya meno (crowns, bridges), au waya za kunyoosha meno (braces)
Hutumika kama suluhisho la haraka kudhibiti ukuaji wa bakteria hatarishi na kuzuia matatizo ya kinywa.
Faida:
Kuzuia ukuaji wa bakteria: Chlorhexidine kwenye Cervitec Fluid huzuia ukuaji wa bakteria ambao husababisha maambukizi ya fizi na kuoza kwa meno.
Ulinzi dhidi ya kuoza kwa meno: Fluoride iliyomo kwenye Cervitec Fluid husaidia kuimarisha enamel ya meno na kupunguza hatari ya kuoza.
Kuondoa harufu mbaya mdomoni :Unaweza kusukutua kuondoa harufu mbaya lakini pia kuua bakteria wanaochagiza utoaji wa harufu mbaya kwa sababu ya kiambata hai chenye ladha ya minti.
Rahisi kutumia: Inaweza kutumiwa kwa urahisi na mtu binafsi au daktari wa meno.
(b)Cervitec Gel:
Hii ni bidhaa ambayo ni ya mfumo wa jeli inayotumiwa kutibu na kudhibiti maeneo yenye hatari ya maambukizi ya bakteria kwenye kinywa na kuzuia kuoza au kutoboka kwa jino.
Matumizi
Matumizi ya Kliniki: Daktari wa meno anaweza kupaka Cervitec Gel kwenye meno, fizi, au maeneo yenye maambukizi ili kutoa tiba na kinga.
Matumizi ya Nyumbani:Chini ya maelekzo ya daktari wagonjwa wanaweza kutumia Cervitec Gel kwa kupaka moja kwa moja kwenye meno au fizi kwa kutumia brashi au vidole.
Inashauriwa kupaka kiasi kidogo mara 1-2 kwa siku, baada ya kusafisha meno, na usinywe wala kula kwa saa moja baada ya kupaka ili kuruhusu dawa kufanya kazi vizuri.
Kutokana na mahitaji yako zipo namna nyingi ya matumizi;
Moja kwa moja kwenye fizi,tishu za ndani ya kinywa ,kwenye ulimi,juu ya jino au kwenye sehemu ya ndani ya meno bandia.
Unaweza kupaka kwenye mswaki maalumu (intradental brush) wa kusafisha kati ya jino na jino au kwa watu wanaotumiwa waya za kunyoosha meno.
Ukaitumia kama dawa ya meno mara moja kwa siku.
Inatumika na kina nani ?
Hutumika kwa wagonjwa walio na matatizo ya fizi au walio na hatari kubwa ya kupata maambukizi ya kinywa kutokana na kutumia vifaa bandia vya meno kama implants, crowns, au dentures.
Hutumika kuimarisha meno yaliyoharibika kutokana na kuoza au madoa madogo yanayoanza kuonekana.
Pia hutumika kwa watu wenye ugonjwa wa mfumo wa kinga (immunocompromised) ambao wako kwenye hatari ya juu ya maambukizi ya kinywa kama vile oral candidiasis.
Faida:
Chlorhexidine husaidia kupunguza na kudhibiti ukuaji wa bakteria hatarishi kwenye fizi na kinywa, kupunguza uvimbe na maumivu kwenye fizi.
Fluoride inasaidia kuimarisha enamel ya meno, hivyo kusaidia kupunguza hatari ya kuoza kwa meno.
Kupunguza na kuondoa harufu mbaya kinywani
Kutuliza maumivu: Cervitec Gel inaweza kusaidia kutuliza maumivu kwenye fizi au maeneo yaliyoathiriwa na maambukizi.
Ulinzi wa kudumu: Matumizi ya mara kwa mara ya gel hii yanaweza kutoa ulinzi wa muda mrefu dhidi ya kuoza kwa meno na magonjwa ya fizi.
Faida za Jumla za Cervitec Fluid na Gel:
Kingamwili dhidi ya magonjwa ya kinywa
Kuimarisha meno
Bidhaa hizi zinaweza kutumiwa na daktari au nyumbani baada ya maelekezo.
Ulinzi maalum kwa wagonjwa wenye vifaa vya meno kama implants au braces .
Zinafaa kutumika kwa matibabu mbalimbali kama magonjwa ya fizi, meno yaliyo kwenye hatari ya kuoza, na hata wagonjwa wenye kinga hafifu dhidi ya maambukizi ya kinywa.
Namna ya Kuishi Kipindi cha Matibabu:
Kufuata maelekezo ya daktari wa meno: Ni muhimu kutumia dawa hizi kama ilivyoelekezwa na daktari wa meno.
Usitumie zaidi ya inavyoshauriwa.
Hakikisha unasafisha meno na kuondoa mabaki ya chakula kwa kutumia floss kabla ya kutumia Cervitec Fluid au Gel.
Epuka kula au kunywa mara baada ya kutumia dawa,subiri angalau dakika 30 kabla ya kula au kunywa ili kuruhusu dawa kufanya kazi vizuri.
Kudumisha ratiba ya miadi ya meno,hakikisha unahudhuria miadi yako ya mara kwa mara kwa daktari wa meno ili kufuatilia maendeleo yako na kuhakikisha tiba inafanya kazi ipasavyo.